GARY CAHILL ADAI KUMTEGEMEA JOHN TERRY KWENYE UNAHODHA WAKE

NAHODHA mpya wa Chelsea, Gary Cahill amesema kuwa staa wa zamani wa timu hiyo, John Terry ndiye atakuwa mtu wa kwanza kumpigia simu pindi mambo yatakapokuwa yanamuwia magumu katika kibarua chake.

Cahill ndiye msimu uliopita alishika nafasi hiyo kwa muda mrefu baada ya Terry kupunguziwa majukumu uwanjani.
Hivi karibuni kocha wa timu hiyo, Antonio Conte alithibitisha kuwa Cahill ndie takayebeba jukumu hilo muda wote baada ya Terry kwenda kujiunga na Aston Villa.

Akizungumza kupitia tovuti ya klabu hiyo baada ya kutangazwa rasmi, Cahill amesema kuwa mara zote amekuwa akiitafakari kazi hiyo ya unahodha na wachezaji ambao wamewahi kuifanya.

“Wakati nikikua, muda wote nilikuwa nawatazama wachezaji wenye uzoefu ili kuona kile ambacho wanakifanya na kwanini wanafanya hivyo,” alisema sta huyo.


“Lakini pamoja na hilo, hakuna mfano mzuri kama John na ilikuwa ni bahati kucheza chini ya unahodha wake kwa miaka mingi,” aliongeza nyota huyo.

No comments