GENEVIEVE NNAJ AVURUGA AKILI YA RAPA PHYNO KIMAPENZI

GENEVIEVE Nnaj ambaye ni staa wa filamu za maigizo nchini Nigeria, ameripotiwa kuvuruga akili ya rapa Phyno aliyeapa kuwa nae siku moja katika maisha yake.

Phyno alisema kwamba kumpata Genevieve ni moja kati ya ndoto zake kubwa kwenye maisha yake ya nje ya masuala ya muziki.

“Niweke wazi tu kuwanampenda Genevieve na ikiwa nitafunga nae ndoa nitakuwa nimetimiza kitu kikubwa kwenye maisha yangu,” alisema staa huyo.

Katika albamu yake ya “No Gots” na “No Glory”, rapa huyo ameweka wazi kuvutiwa kimapenzi na Genevieve.


Phyno amekuwa akizungumza bila kuficha hisia zake kwa Genevieve hata anapokuwa kwenye kamera za waandishi wa habari.

No comments