GIGY MONEY ADAIAMEACHA MAMBO YA KITOTO

VIDEO Queen anayezipendesha video za wasanii Bongo, Gift Stanford “Gigy Money” amefunguka na kusema kwa sasa amekuwa mtu nzima hivyo hawezi kuishi maisha kama ya zamani ya kufanya matukio.

Gigy Money alisema sasa umri wa ukubwa umefika hivyo hawezi kwenda na matukio kama aliyoyafanya zamani kwani ule ulikuwa utoto tu.

“Sasa nimekua, najua nini maana ya maisha hivyo siwezi kuyafanya mambo ya kitoto niliyokuwa nafanya zamani kwa sababu nahitaji muda mwingi wa kutengeneza maisha,” alisema Gigy.


Aliongeza kuwa anatambua thamani ya kazi anayohifanya ya kuzipendezesha nyimbo za wasanii wenzake hivyo atahakikisha anakaza buti ili aweze kutimiza malengo yake.

No comments