GUARDIOLA ASEMA ANATAMANI KULETA BEKI MWINGINE MANCHESTER CITY

KOCHA wa Manchester City, Pep Guardiola, amekiri kuwa angependa kusajili beki mwingine, japo ana furaha na hali ya kikosi chake kwa sasa.

Akizungumza kabla ya mchezo wa mwisho wa ‘pre-season’ dhidi ya Tottenham, Guardiola alisema kuwa, ameridhishwa na upana wa kikosi chake hivi sasa.

"Nina furaha na John Stones, Vincent Kompany na Nicolas Otamendi.

"Kwa sasa hatutakiwi kusajili sana, japo tulifanya hivyo kwa sababu tulitakiwa kuongeza idadi kubwa ya wachezaji kwenye kikosi chetu.

"Lakini kama nikipata nafasi ya kusajili zaidi, ningependa kuongeza beki mwingine wa kati," alisema Guardiola.

Mpaka sasa City wametumia pauni milioni 200 za usajili, huku pauni 120 akizitumia kusajili mabeki tu.

No comments