GUARDIOLA AWEKA WAZI "SAMIR NASRI ANAJIANDAA KUSEPA MANCHESTER CITY"

KOCHA wa Man City, Pep Guardiola amekiri akisema kwamba staa wake,  Samir Nasri  anajiandaa kuondoka kwenye kikosi chake licha ya  kufanya vizuri katika mechi za majaribio za kujiandaa na msimu ujao.

Nasri  aliutumia msimu ukliopita akikipiga kwa mkopo katika timu ya  Sevilla  nchini Hispania, lakini cha kushangaza akaweza kuwamo kwenye kikosi cha Man City kilikuwa ziarani nchini Marekani   na akaweza kutamba kwenye michuano ya Mabingwa wa Kimataifa.

Kiungo huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka  30 alitokea benchi katika mchezo wa juzi ambao waliondoka na ushindi wa mabao  3-0  dhidi ya  Tottenham, lakini  Guardiola anasema kwamba nyota huyo ataondoka kabla ya msimu wa Ligi Kuu ujao haujaanza.

"Tulitaka kuwa naye katika maandalio ya msimu uliopita lakini akaamua kwenda  Sevilla," alisema Guardiola.
“Anafahamu jinsi hali ilivyo  kutokana na kwamba tuna wachezaji wengi katika safu ya viungo.Na sio yeye tu yuko kama vile Mangala ni uamuzi wake ni kama ulivyo kwa makocha,”aliongeza kocha huyo.

Alisema kwamba  wataendelea kumjali katika kipindi watakuwa naye  na akasema kwamba anavyojituma ni kama mchezaji ambaye wataendelea kuwa naye.

No comments