HARAKATI ZA NYOSHI EL SAADAT USIPIME


Aliyekuwa rais wa FM Academia Nyoshi el Saadat amesema anakuja na ‘project’ nyingi za muziki na za nje ya muziki ambazo anaamini zitaendelea kuipandisha juu heshima yake.

Nyoshi ambaye ameachana na FM Academia, ameiambia Saluti5 kuwa kwa sasa hawawezi kuweka wazi mipango yake hadi hapo utakapowadia wakati sahihi.

Juzi Nyoshi alikuwa bize na kundi la vijana wengi wakiwemo wanamuziki na wasio wanamuziki (kama anavyoonekana pichani juu). Nini kinafuata? Tuvute subira.

No comments