HATIMAYE ARSENAL 'YAMTIA' MKONONI ALEXANDRE LACAZETTE KWA PAUNI MIL 44


Arsenal imefikia makubaliano na klabu ya Lyon kwajili ya kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette kwa ada ya pauni milioni 44 itakayoweka rekodi mpya ya usajili wa bei mbaya Emirates.

Ada hiyo itaipuku ile ya pauni milioni 42.5 iliyolipwa na Arsenal wakati ilipomsajili Mesut Ozil kutoka Real Madrid mwaka 2013.

Usajili wa Lacazette utakamilika ndani ya saa 48 baada ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kusafiri kwenda London kwaajili ya vipimo vya afya.

Arsenal ilijaribu bila mafanikio kumsajili Lacazette msimu uliopita ambapo ofa yao ya pauni milioni 29 ilipigwa chini.

Msimu huu ikarejea tena na ofa ya pauni milioni 39.5 ambayo nayo ilikataliwa kabla ya kuiboresha na kufikia makubaliano na mmiliki wa Lyon, Jean-Michel Aulas kwa dau la pauni milioni 44.No comments