HATIMAYE JAVIER HERNANDEZ "CHICHARITO” ANAREJEA PREMIER LEAGUE


West Ham imethibitisha kuwa imefikia makubaliano na Bayer Leverkusen ili kumsajili mshambuliaji  wa zamani wa Manchester United Javier Hernandez "Chicharito".

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 atasafiri kwenda London wikiendi hii kwaajili ya vipimo vya afya kabla ya kukamilisha usajili wake wa pauni milioni 16.

Huu unakuwa ujio wa mara nyingine tena kwenye Premier League kwa nyota huyo wa Mexico baada ya hapo nyuma kuitumikia Manchester United kwa misimu minne na kushinda mataji mawili ya Premier League.

No comments