HATIMAYE LULU AANIKA KINACHOMKONDESHA

MSANII wa filamu nchini, Elzabeth Michael "Lulu" ameweka wazi kuwa mazoezi ya viungo pamoja na kushinda akila matunda pekee ndiyo sababu inazofanya mwili wake kupungua.

Akizungumza na saluti5, mrembo huyo alisema kuwa ameamua kupunguza mwili kwa makusudi na kwamba kila siku anashinda akila matunda na kufanya mazoezi magumu ya viungo.

“Watashangaa sana kunona napungua lakini nafanya hivi sijashauriwa na mtu ni kuweka tu mwili wangu sawa, nafanya sana mazoezi naenda gym kila siku na kuhakikusha muda mwingi nashinda kwa kula matunda kuliko chakula," alisema.


Aidha mrembo huyo aliongeza kwa kusema kuwa watu wanatakiwa kufanya mazoezi kwa wingi kujenga miili yao na si kusubiri mpaka wandikiwe au washauriwe na madaktari ndio wafanye mazoezi.

No comments