HATIMAYE MANCHESTER UNITED YAMCHEFUA MOURINHO


GAZETI la The Sun limesema kuwa Jose Mourinho 'The Special One' hafurahishwi na kasi ndogo ya Makamu Mwenyekiti Mtendaji wa Manchester United, Edward Gareth “Ed” Woodward katika soko la usajili wa kiangazi hiki. 

Beki wa kati Victor Lindelof ni mchezaji pekee ambaye United imemsajili hadi sasa akitokea Benfica ya Ureno kwa dili la pauni milioni 39.6.

Mourinho anataka kumaliza haraka usajili wa nyota wengine watatu walio mstari wa mbele katika orodha ya mastaa anaowataka kuimarisha kikosi chake ambao ni straika wa Real Madrid, Alvaro Morata, winga wa Inter Milan, Ivan Perisic na kiungo wa Chelsea, Nemanja Matic.

The Sun limepasha kuwa kocha huyo Mreno anataka nyota wote hao kuwa nao ndani ya ndege kwa safari ya kambi ya maandalizi ya msimu mpya nchini Marekani ndani ya kipindi kisichopungua wiki moja kutoka sasa.

Hata hivyo, inaonekana kuwa uharaka anaotaka Mourinho hauwezekani kutokana na Ed Woodward kukwama kupata saini za nyota hao kutokana na vikwazo vya klabu zao.

No comments