EVERTON inatarajiwa kufanya usajili wa kushtua wiki hii kwa kumrejesha Goodison Park straika wake wa zamani, Wayne Rooney na Olivier Giroud wa Arsenal atamfuata nahodha huyo wa Manchester United.

Vyanzo kutoka klabu zote mbili vimepasha kuwa Everton itamtwaa Rooney kwa usajili huru, lakini itaendelea kumlipa mshahara wake wa sasa wa pauni 250,000 kwa wiki, huku ikitenga pauni milioni 20 kama ada ya kumtoa Giroud Emirates.

Rooney, 31, anarudi Everton alikoondoka miaka 13 iliyopita, baada ya kukosa nafasi United na ameondolewa katika kikosi kitakachokwenda Marekani Jumapili kwa ziara ya maandalizi ya msimu.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac