HATIMAYE NYEMAR AKUBALI KUMWAGA WINO PSG

STRAIKA wa Barcelona Neymar, 25, amekubali kusaini mkataba wa miaka mitano kujiunga na Paris Saint-Germain na huenda akakamilisha uhamisho wa pauni milioni 197 wiki hii.  

Taarifa  zilizojili jana katika gazeti la Marca nchini Hispania tayari Mbrazil huyo licha ya kuwa hajaukea wazi uongozi wa klabu hiyo, lakini staa huyo ameshaanza kuwaaga  nyota wenzeke kwamba anakwensda kujiunga na matajiri hao wa Ufaransa.

Gazeti hilo lilikwenda mbali zaidi likieleza kuwa pia klabu ya PSG watawapa Barcelona Angel Di Maria, 29, kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Neymar, ili kupunguza kodi ya kutengua kifungu cha uhamisho cha mchezaji huyo wa Brazil.


Iwapo Neymar ataondoka, Barcelona wataamua kuwawinda wachezaji watatu kutoka EPL- Philippe Coutinho, 25, wa Liverpool, Eden Hazard, 26, wa Chelsea, na Delle Alli, 21 wa Tottenham ili kuziba pengo.

No comments