HATIMAYE SIMBA DAY KUFANYIKIA MKOANI ARUSHA

MABOSI wa Simba kwa kuthamini thamani ya mashabiki wao wameamua kabla ya msimu huu kuwepo na tamasha lao la kila mwaka siku chache kabla ya Ligi kuanza "Simba Day" kuifanyia mkoani Arusha.

Wekundu wa Msimbazi wanatarajia kuweka kambi ya timu ya maandalizi kati ya Moroco na mkoani Morogoro kuanzia Julai 9.

Mmoja wa viongozi wakuu ameiambia saluti5 kuwa wamekubaliana kati ya Agosti 4 kufanya Simba Day ndogo Arusha kutambulisha kikosi chao msimu ujao kabla ya kurejea Dar kuadhimisha tarehe yenyewe Agosti 8.


“Tunaraji kuwa na Simba Day ndogo Arusha ikiwa ni baada ya wachezaji wetu kujifua ndani ya mwezi mzima kwenye kambi itakayokuwa nje ya nchi, Morocco au hapahapa nchini mkoani Morogoro,” alisema kiongozi huyo.

No comments