HERRERA ASEMA ATAHAKIKISHA DE GEA HAONDOKI MANCHESTER UNITED


Kiungo wa Kihispania, Ander Herrera anasema atafanya kila awezalo kuhakikisha   David de Gea anabakia Manchester United badala ya kujiunga na Real Madrid.

De Gea, kipa namba moja wa Hispania, anawaniwa kwa udi na uvumba na Real Madrid inayotarajiwa kuwepa mezani pauni milioni 60, lakini United imeshaweka wazi kuwa kipa huyo hayupo sokoni.

Herrera amesema: "De Gea ni kipa bora na ningependa kuendelea kuwa nae pamoja Manchester United na hivyo nitafanya kila niwezalo kumshawishi ili asiondoke".


No comments