HUSSEIN NYIKA WA YANGA ATISHIA KUSHITUA ULIMWENGU MWISHONI MWA WIKI HII

MWENYEKITI wa kamati ya usajili ya Yanga, Hussen  Nyika amesema bado wapo katika harakati za usajili na kwamba ukimya wao kwa sasa wanafanya uchaguzi juu ya nyota wapya wanaowataka lakini mwisho wa wiki hii watashtua ulimwengu wa soka.

Nyika alisema bado hawajamaliza usajili na kwamba bado kuna nafasi nne wanazipigia hesabu ambapo majina makubwa ndiyo wanayoyafanyia kazi kwa sasa.

Nyika ambaye ni mzoefu katika mambo ya usajili, amesema sehemu kubwa ambayo wanataka watulize akili ni kupata viungo wa kazi katika kuiboresha timu yao, kazi ambayo weanaifanya kwa ushirikiano mkubwa na benchi la ufundi la timu yao chini ya kocha Geogre Lwandamina.

Bosi huyo alisema kwa sasa hataki kutaja majina ya viungo wanaowapigia hesabu lakini mambo yakikamilika waki hii watashtua ulimwengu wa soka kwa kuleta vifaa vya maana.

Hata hivyo saluti5 imedokezwa kwamba Yanga inaweza kushtua ulimwengu kwa kumshusha kiungo wa Mbabane Swallows, Kabamba Tshishimbi, Raphael  Daudi na kisha kumuongezea mkataba mkongwe Thaban Kamusoko ambaye tayari yupo nchini.

“Tunafanya mambo kimakini, kawaida yetu mambo yanapokamilika ndio tunayaweka wazi tunapokuwa kimya mjue kwamba tunafanya kazi kimyakimya tukishirikiana na makocha wetu,”alisema Nyika.


“Tunatafuta viungo mahususi kwa mahitaji ya timu yetu, safari hii tumedhamiria kuondoa mapungufu katika eneo hilo tukikamilisha mapema huenda wiki hii tutashtua ulimwengu wa soka."

No comments