IBRAHIM AJIB AUKUBALI "MUZIKI" WA YANGA

MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga, Ibrahim Ajib ameonekana kuukubali muziki wa Yanga kutokana na mazoezi aliyoyafanya kwa muda mfupi, huku akisema moja ya malengo yake msimu ujao ni kuhakikisha timu hiyo inatetea ubingwa wake.

Ajib amejiunga na Yanga katika dirisha hili la usajili akitokea Simba na tayari ameanza mazoezi na timu hiyo.

Akiongea na saluti5, Ajibu alisema Yanga inaweza kutetea ubingwa wake na anataka kuwa sehemu ya mafanikio ya klabu hiyo.

“Litakuwa jambo muhimu sana na la maana kama Yanga itatea ubingwa wake na mimi kuwa sehemu ya mafanikio,” alisema Ajib.

Aidha, alisema anaamini usajili uliofanywa na timu hiyo utawapa mafanikio msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara pamoja na michuano ya kimataifa.


Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), tayari limetoa ratiba ya msimu ujao ambao utaanza Agosti 26, mwaka huu na Yanga itafungua dimba kwa kucheza na Lipuli ya mjini Iringa kwenye uwanja wa Taifa Agosti 27.

No comments