IBRAHIMOVIC ANAPONA KWA HARAKA SANA ...MAN UNITED 'KUMPA' MKATABA MPYA, KUREJEA UWANJANI OKTOBA


ZLATAN IBRAHIMOVIC anapona kwa haraka kuliko ilivyotegemewa na huenda akalambiswa mkataba mpya Manchester United.
Ibra, 35, aliumia vibaya goti katika mchezo wa Europa League dhidi ya Anderlecht mwezi April, na alitarajiwa kuwa nje ya dimba hadi mwaka mpya.
Lakini sasa mkongwe huyo anatarajiwa kuwa tayari kwa kurejea uwanjani mwezi Oktoba ambapo Manchester United inasubiri kwa hamu kuona mandeleo yake ili imsainishe mkataba mpya.
Ilihofiwa kuwa hatma ya soka la Ibra imewadia ambapo United ilimtema rasmi mwezi uliopita na kusitisha kipengele cha kuongeza mwaka wa pili kwenye mkataba wake.
Licha ya kuachwa na United lakini Ibrahimovic aliendelea kubaki Manchester akiwa anaendelea kuukarabati mwili kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo - Carrington.
Madaktari wa United wameduwazwa na maendeleo ya nyota huyo wa Sweden huku ikiaminika kuwa Jose Mourinho atakuwa tayari kumpa mkataba mpya iwapo atarejea uwanjani mapema.

No comments