INI EDDO AFANYIWA UPASUAJI ILI KUONGEZA UKUBWA WA MAKALIO

STAA wa filamu nchini Nigeria, Ini Eddo ameripotiwa kufanya upasuaji ili kuongeza ukubwa wa makalio yake na kutengeneza mvuto zaidi.

Rafiki wa karibu wa staa huyo amesema kuwa imetumika naila mil 5 ili kufanikisha upasuaji huo.

Mwanzoni alikuwa akikanusha kufanyiwa upasuaji huo kabla ya rafiki yake wa karibu kufichua taarifa hiyo kwenye vyombo vya habari.

Imekuwa tabia kwa mastaa wa filamu nchini Nigeria kufanya upasuaji huo ili kuongeza mvuto kwa mashabiki wao na watu wanaowatazama.


Mwimbaji wa Marekani, Jennifer Lopez anatajwa kuwa chanzo cha masta wengine kuingia kwenye mkumbo huo baada ya upasuaji wake kufanikiwa miaka kadhaa iliyopita.

No comments