INTER MILAN ‘YAHITIMISHA’ TETESI ZA IVAN PERISIC KWENDA MAN UNITED


Mbio za Manchester United kuwania usajili wa Ivan Perisic, zinaweza kuwa zimefika ukingoni baada ya kocha wa Inter Milan, Luciano Spalletti kusema kwa sasa hataki tena winga huyo apigwe bei.
Spalletti amesema: "Kuna jambo unaweza kuwa unalifahamu tangu dirisha la usajili linapofunguliwa, lakini kusiwepo na maendeleo yoyote na kwa hali hiyo basi, kwangu mimi nasema mjadala umefungwa.
"Nitapinga kwa nguvu zangu zote mauzo ya Perisic iwapo ofa italetwa mezani".
Manchester United bado imeshindwa kufika bei ya pauni milioni 45 inayotakiwa na Inter Milan na sasa makamu mtendaji wa United, Ed Woodward yupo kwenye shinikizo kubwa la kutekeleza utashi wa Jose Mourinho ambaye anataka kusajili wachezaji wawili zaidi.

No comments