INTER MILAN YAZIKATA MAINI LIVERPOOL NA ARSENAL

KAMA ingekuwa wanajua kuwa wanachokifanya kingekuwa kazi bure, basi Liverpool na Arsenal wasingesumbuka kumwania nyota mmoja kwa muda mrefu sasa.  

Licha ya kwamba walikuwa wametenga kitita kikubwa, lakini Liverpool wameshindwa kuinasa saini ya mchezaji mmoja mzuri sana wa kikosi cha Nice ya Ufaransa, Dalbert Henrique.

Vyanzo vya habari vinasema kwamba Liverpool wanamtaka mchezaji huyo lakini Inter ni kama wameiwahi na wakati wowote watamalizana.

“Wakala wangu amemaliza kila kitu. Ni kweli kwamba walikuwa wananitaka sana watu wa Liverpool lakini naona kama sasa nitakwenda Italia,” amesema nyota huyo raia wa Brazil.

Liverpool wamekuwa wakiamini kwamba wachezaji raia wa Brazil wamekuwa mahiri sana uwanjani na siku zote huwa wanatolea macho hadi dakika ya mwisho.

Timu nyingine ambayo ilikuwa inamwinda mchezaji huyo mahiri ni Arsenal ambayo inadaiwa kuwa ilishapeleka ofa ya Euro mil 20 kuinasa saini ya nyota huyo lakini ofa hiyo ikapigwa chini.


Kocha Arsene Wenger aliwahi kusema kwamba kiungo mshambuliaji huyo ana vitu vingi ambavyo anataka kuvihamishia katika timu yake.

No comments