ISTANBUL BASAKSEHIR SASA YATHIBITISHA KUMNYAKUA GAEL CLICHY

UVUMI una kikomo chake na muda mwingine huvuma sana na mwisho hugeuka ukweli au uongo.

Kwa wiki nzima kumekuwa na uvumi kwamba beki wa kushoto wa zamani wa Manchester City, Gael Clichy atajiunga na klabu ya Uturuki ya Istanbul Basaksehir.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 hakupewa mkataba mpya Etihad baada ya mkataba wake kumalizika mwisho wa msimu wa 2016/17.

Na habari mpya zikasema kwamba klabu hiyo imethibitisha kwenye mitandao ya kijamii kwamba atafanyiwa uchunguziwa kimatibabu kabla ya kutia saini mkataba Ijumaa.

Clichy alijiunga na City kutoka Arsenal mwaka 2011 na alishinda mataji ya Ligi ya Premier mara mbili na Kombe moja la EFL akiwa na klabu hiyo.

Maelezo zaidi kuhusu kutua kwake Uturuki hayajatolewa lakini taarifa uturuki zinasema huenda beki huyo atalipwa Euro Mil 3 kila siku na kwamba mkataba wake ni wa miaka mitatu.

Clichy atajiunga sana na mshambuliaji wa zamani wa City na Arsenal, Emmanuel Adebayor ambaye alijiunga na Istanbul Basaksehir mwezi Januari.

Klabu hiyo ilimaliza ya pili ligi Kuu ya Uturuki msimu uliopita ambapo Adebayor aliwafungia mabao sita kwenye Ligi Kuu.

Yeye mwenyewe alipoulizwa akasema kwamba huenda habari hizo zikiwa kweli lakini pia haitakuwa jambo la ajabu kwake kuhamia kwenye Ligi Kuu ya Uturuki.


“Kwangu mimi najua kwamba naweza kuhamia kweli Uturuki na haiwezi kuwa jambo la ajabu sana kule kuna Ligi nzuri sana na unaona wachezaji wengine wakubwa wanakimbilia kule,” amesema.

No comments