Habari

IVAN PERISIC ANAYEWANIWA NA MANCHESTER UNITED AWASILI KWENYE ZIARA YA MAANDALIZI YA MSIMU MPYA

on

Winga anayewaniwa na Manchester United  Ivan Perisic, amekanyaga ardhi ya China akiwa na wachezaji wenzake wa Inter Milan tayari kwa ziara ya maadalizi ya msimu mpya.
United  ilikuwa inaamini itamnyakua nyota huyo wa kimataifa wa Croatia kwa pauni milioni 44 huku  Perisic mwenyewe akiwa na uchu wa kutua Old Trafford katika dirisha hili la usajili.
Hata hivyo usajili huo umezidi kubakia njia panda baada ya Perisic kujumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji wa Inter waliosafiri kwenda china.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *