J FOUR SUKARI: NASHIRIKI SHOW ZA TWANGA PEPETA ILI KIPAJI CHANGU KISIPOTEE


Kwa lugha nyingine unaweza kusema msanii huyu amekiri kuwa kwake yeye Twanga Pepeta ndiyo sehemu pekee ya kuokoa kipaji chake.

Huyo ni mwimbaji na rapa Jumanne Seseme “J Four Sukari” wa TOT Band ambaye amekiri kuwa ‘hakauki’ kwenye maonyesho ya Twanga Pepeta ili kuokoa kipaji chake.

J Four ambaye alikuwa mmoja wa wasanii waliopunguzwa Twanga na hatimaye kujiunga na TOT, amesema bendi yake ina uhaba wa maonyesho na hivyo akikaa nyumbani kipaji chake kitapotea.

“Nashiriki maonyesho mengi ya Twanga Pepeta ili kulinda kipaji changu, mwanamuziki ni sawa na mchezaji mpira bila mazoezi uwezo wako unapungua,” alisema J Four.

No comments