JADON SANCHO WA MAN CITY AZIINGIZA VITANI ARSENAL NA TOTTENHAM

VIGOGO vya premier, Arsenal na Tottenham Hotspur wamo katika kupigana vikumbo vya kuimarisha vikosi vyao msimu huu kwa kumwania Jadon Sancho.

Sancho kwa sasa hayumo katika kikosi cha Manchester City kilichoko nchini Marekani kwa ajili ya kucheza mechi za awali kwa ajili ya kujipima uwezo kabla ya kuanza kwa msimu wa premier.

Kocha Pep Guardiola hata hivyo bado hajaweka bayana hatma ya Sancho ambaye hajaongezewa kandarasi ya kubakia kikosini.

Kinda huyo mwenye umri wa miaka 17 ni miongoni mwa wanandinga vijana waliolelewa katika kituo cha kukuzia vipaji cha Manchester City ambaye Tottenham wanamwangalia kwa jicho la kumwamini kupita kiasi.

Hata hivyo taarifa kutoka ndani ya Manchester City zinasema kuwa uongozi wa juu bado unataka kuketi na sancho kwa ajili ya kumuongezea kandarasi ya miaka mitatu na kupanga kumlipa mshahara wa pauni mil 30 kwa juma.

Hatua ya City kutaka kumbakiza sancho inatokana na ukweli kuwa ndie aliyeisaidia timu ya taifa ya England kutwaa ubingwa wa dunia kwa timu za vijana hivyo haipaswi kumuacha.


Lakini Arsenal nao wamesikia taarifa za kutoongezwa mkataba kwa sancho hivyo nao wameamua kutupa ndoano ya kumwania kinda huyo.

No comments