JAHAZI MODERN TAARAB KAMBINI KWA AJILI YA NYIMBO MPYA

MAGWIJI wa mipasho, Jahazi Modern Taarab wiki hii wanatarajiwa kuingia kambini kwa ajili ya kupika vibao vipya vitatu, kimoja kikiwa ni cha bosi wao ‘kichefuchefu’, Aboubakar Soud ‘Prince Amigo’.

Mkurugenzi wa wasanii wa bendi hiyo, Ally Jay aliieleza saluti5 kuwa, kambi hiyo itakuwa ni ya wiki mbili ambapo watakapomaliza kupika vibao hivyo, moja kwa moja wataingia kuvirekodi.

“Tuliachia vibao vya utangulizi vya ‘Nataka Jibu’ na ‘Jicho la Mungu Halilali’, sasa tumeona ni muda mwafaka kuendelea na matayarisho ya albamu yetu mpya,” alisema Ally Jay ambaye ni mkali wa kinanda cha taarab anayesumbua Bongo.


Aliwaomba mashabiki na wapenzi wao wote kukaa mkao wa kusubiri ujio wa kazi zao hizo tatu mpya ambazo anaamini zitakuwa funika bovu kutokana na namna walivyojiandaa nazo vya kutosha.

No comments