Mlipuko wa burudani unategemewa kutokea katika onyesho bab kubwa lililopewa jina la ‘Usiku wa kucharuka Kipwani na Singeli’ litakalofanyika ndani ya Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Taarifa kutoka waandaaji wa onyesho hilo zinasema kuwa, shoo hiyo itapigwa Agosti 5, huku bendi za Jahazi Modern Taarab na Zanzibar Stars Modern Taarab zikirarajiwa kukutana jukwaa moja.

Mbali na bendi hizo, pia kutakuwa burudani kutoka kwa Khadija Kopa, Khadija Yussuf, Hanifa Maulid, Dullah Makabila na Kivurande Junior.

“Kiingilio katika shoo hiyo kitakuwa ni sh. 7,000 ambapo watakaohudhuria watafaidi mambo mengi matamu ya burudani, vikiwemo vibao vipya kutoka kwa kila bendi na kila msanii aliyealikwa,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa shoo hiyo imeandaliwa maalum kwa ajili ya kutii maombi ya mashabiki wengi wa Temeke walioomba kutayarishiwa onyesho kubwa ili kujiburudisha na kukosha nafsi zao ipasavyo.

USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac