Habari

JAMAL MNYATE ASEMA “BADO NIPONIPO SIMBA SC”

on

WAKATI Pastory Athanas
amejiunga na Singida United kwa mkataba wa miaka miwili, winga mwingine wa Simb,a
Jamal Mnyate amesema bado yupoyupo Simba.
Jana timu hiyo ya Singida
imemtambulisha Athanas ambaye Simba walimsajili kutoka Stand United ya
Shinyanga katika usajili uliopita wa dirisha na akawa hana nafasi ya kutosha
katika wekundu hao wa Msimbazi.
Lakini kwa upande wake Mnyate
ambaye naye majeruhi yalimfanya akose kupata nafasi katika kikosi cha kwanza
cha Simba, amefunguka na kusema bado ataendelea kuweko kwenye klabu hiyo
kutokana na kuwa na mkataba na timu hiyo.
Mnyate alisajiliwa na Simba
kutoka timu ya Mwadui kwa mkataba wa miaka miwili lakini tangu aliposajiliwa
alifanikiwa kucheza mechi kadhaa kutokana na mara nyingi kuwa anasumbuliwa na
majeruhi.
“Kwa hivi sasa ni ngumu kusema
msimu ujao nitakuwa wapi kwasababu bado nina mkataba wa mwaka mmoja na Simba, kikubwa mimi nawasikiliza wao waajili wangu watakavyonambia kuhusu hatima
yangu,” alisema.
Mnyate alisema hawezi
kuzungumza chochote kwa sasa kutokana na kuwa bado yupo chini ya mkataba
angekuwa huru kusema msimu ujao angeenda timu gani.
Aidha Mnyate amewapongeza
viongozi wake kwa usajili walioufanya kwa kuwarudisha wachezaji wao wa zamani
kama Emmanuel Okwi, Shomary Kapombe ambao walikuwa tishio Ligi Kuu.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *