JAMAL MWAMBELEKO ACHEKELEA KUREJEA KWA OKWI MSIMBAZI

BEKI mpya wa Simba, Jamal Mwambeleko amechekelea kurejea kwa straika Emmanuel Okwi na kusema kuwa kikosi cha wekundu hao kitakuwa cha mfano.

Mwambeleko amesema kuwa anaamini ujio wa Okwi utaongeza ushindani katika kikosi chao kinachopambana kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara huku pia kikikabiliwa na michuano ya kimataifa mwakani.

“Ni mchezaji mzuri na anaongeza ushindani kwa sababu kila mmoja anatamani kuona anakuwa kwenye kikosi cha kwanza.”


“Naweza kusema Okwi ni mchezaji ambae hapotezi nafasi kama akiipata, hivyo Simba ya msimu ujao mtaiona itakuwa ya mafanikio zaidi, hata michuano ya kimataifa ina nafasi ya kufika mbali,” alisema Mwambeleko.

No comments