JAVIER PASTORE AKIRI KUWANIWA NA CHELSEA NA MAN CITY

NYOTA wa klabu ya PGS, Javier Pastore amekiri tetesi za kuwaniwa na timu kadhaa za Primier lakini Chelsea na Manchester City ndiyo wanaoongoza mbio hizo.

Lakini matajiri wa jiji la London, Chelsea wameongeza kasi ya kumwania kwa ajili ya kutua darajani chini kocha Antonio Conte.

Awali Pastore amekuwa akihusishwa na tetesi za kutaka kutua kwa washika mitutu wa jiji la London na Arsene Wenger ameweka mezani ofa kwa ajili yake.

Lakini kocha Antonie Conte inasemekana ameingilia kati dili hilo na anapambana kuhakikisha kiungo huyo antua katika kikosi cha Stamford Bridge.

Akinukuliwa, Pastore amesema ndoto zake za kutua Emirates zinaweza kuyeyuka kwa sababu Conte ameongeza kasi ya mazungumzo.

“Nimekuwa nikisikia malengo ya Conte kwangu na kadri ninavyotambua mpango uko hivyo.”

“Ni kati ya makocha wazuri duniani wanaovutia kufanya kazi nao. Kila mchezaji anaota ndoto ya kufundishwa na mwalimu wa mfano wake”.

“Kwa nyakati tofauti nimekuwa nikifundishwa na makocha wengine.

Kama kuna siku inatokea napata nafasi ya kufanya kazi chini yake nitakuwa na furaha kubwa.

“Lakini kwa sasa bado nipo PSG. Najisikia furaha kuwa hapa hakuna tatizo kuwa hapa”.

“Kucheza katika timu inayoshiriki Ligi ya Mabingwa ni kati ya malengo yangu pia. Kila mchezaji anaota mafanikio kama hayo”.

Ninataraji kuwa katika kiwango hicho cha mafanikio, ninaamini kuna siku nitafikia hatua hiyo niswala la kusubiri kuona,”alisisitiza Pastore.

No comments