JERAHA LA KIWIKO KUMKOSESHA DJOKOVIC MICHUANO YA US OPEN

BINGWA mara 12 wa mataji makubwa ya mchezo ya Grand Slam, Novak Djokovic,  anatarajia kuyakosa mashindano ya Us Open mara baada ya kupata majeraha ya kiwiko ambayo yatamuweka nje kwa zaidi ya mwezi mmoja.

Djokovic, mwenye umri wa miaka 30 na bingwa wa mashindano ya Wimbledon, amesema anaumia kuyakosa mashindano hayo makubwa ya mchezo wa tenesi duniani.

"Itanichukua muda hadi hali yangu kutengamaa," alisema Djokovic, alipokuwa akifanyiwa mahojiano na kituo cha habari cha BBC.

Djokovic hakuwa na msimu mzuri mwaka uliopita, kutokana na kuandamwa na majeraha ya mara kwa mara, ambayo yalisababisha ashuke katika viwango vya ubora katika mchezo wa tenisi kwa upande wa wanaume.

Hivi sasa mkali huyo anashika nafasi ya nne akiwa nyuma ya Roger Federer, Rafael Nadal pamoja na Mwingereza Andy Murray, anayeshika nafasi ya kwanza.

No comments