JEZI NAMBA 9 ILIVYOMTOA UDENDA LUKAKU OLD TRAFFORD


ROMELU LUKAKU amefichua kuwa alilazimika kuomba ruhusa kwa Zlatan Ibrahimovic kabla kuomba kuvaa jezi No. 9 Manchester United msimu ujao.

Straika huyo tayari amekamilisha uhamisho wake Old Trafford baada ya United kufikia makubaliano ya pauni milioni 75 na Everton wiki iliyopita.

Alivaa jezi No. 10 Goodison Park, ambako alifunga mabao 71 katika michezo 133 baada ya kusaini mkataba wa kudumu akitokea Chelsea mwaka 2014.

Lukaku alisema: "Mara zote huwa namuuliza mama yangu nivae namba gani, na nimekuwa nikicheza na No.10 kwa sababu ‘bethidei’ ya mama yangu ni Oktoba 10, hivyo ni mwezi wa kumi wa mwaka.

"Hiyo ndiyo sababu nilicheza na No. 10. Niliulizia namba tisa kwa sababu mimi ni straika.


"Straika anacheza na No. 9. Ni namba nzuri, na niliomba ruhusa ya Zlatan Ibrahimovic. Ninataka kumshukuru pia kwa kuniruhusu nivae namba hiyo."

No comments