JOEL BENDELA AFICHUA SIRI YA KUKOSEKANA KWA TIMU BORA YA TAIFA

MKUU wa mkoa wa Manyara mheshimiwa Joel Bendera amesema kuwa ni vigumu kupata timu bora ya taifa kwasababu ya kukosekana kwa vituo vya kuendeleza vipaji vya vijana hapa nchini.

Mheshimiwa Joel Bendera ambaye ni mdau wa soka siku nyingi aliyewahi kuifundisha Stars miaka ya themanini alisisitiza kuwa wachezaji wengi wanapata nafasi ya kuchezaa Stars wakiwa na umri mkubwa hivyi ni vigumu kupata kikosi bora chenye ushindi.

“Tutahanga niaka nenda rudi lakini dawa ni kuanzisha vituo vingi vya kuendeleza mchezo wa soka kwasababu nyota wengi wanaingia kikosi cha timu ya taifa wakiwa na umri mkubwa” alisema mdau huyo wa soka.


“Unawezaje kupata mafanikio bila kuwa na msingi bora wa timu ya vihana ndio maana kila wakati tunaishia njiani kwenye michuno mikubwa” alimaliza.

No comments