"JOHN BOCCO AMEZALIWA UPYA SIMBA SC"

UMEWAHI kumuona mtu akiwa mpya? Basi kama hujawahi kumuona mtu wa aina hiyo siku ukibahatika kuiona Simba na kukutana na John Bocco utaona kama amezaliwa upya.

Bocco ametua katika kambi ya Simba nchini Afrika Kusini baada ya kuitumikia timu ya taifa akiwa na wachezaji wenzake wa Simba waliokuwa katika kikosi hicho cha Stars.

Bocco alionekana mwenye furaha ya ajabu akiwa katika jezi nyekundu kwa mara ya kwanza, lakini hata katika mazoezi alionekana mpya, mwenye kasi na morari ya ajabu.

“Huyu jamaa ni kama amezaliwa upya, unamuona anavyopambana kwenye mazoezi na kuonekana na morari kubwa. Nadhani kuna nadhri alikuwa ameweka na sasa ameitimiza,” alisema mmoja wa wachezaji wa Simba kwa utani.


Bocco amejiunga na Simba kwa mara ya kwanza baada ya kuitumikia Azam tangu ianzishwe. Amekuwa nahodha wa Azam kwa muda mrefu na sasa anaingia kwenye timu ambayo anadaiwa kuwa na mapenzi nayo ya miaka mingi.

No comments