JOSE MARA: WATU WA DANSI TUSICHINJE NG’OMBE MZIMA KWA ODA YA MAINI


Mkurungezi wa Mapacha Music Band (Mapacha Watatu), Jose Mara amewataka wanamuziki wa dansi wapunguze majungu na badala yake wajikite kwenye kufanya kazi zenye tija sokoni.

Akiongea na Saluti5, Jose Mara akafafanua kuwa sasa hivi wanamuziki wengi wamepunguza bidii ya kufanya kazi na wamehamishia nguvu zao kwenye majungu.

Amesema inafika wakati msanii wa dansi anakwenda kutambulisha kazi yake mpya radioni lakini anapofika huko anasahau kile kilichompeleka na kutumia muda wake mwingi kuteta na kusengenya wasanii wenzao.

“Muziki wa dansi kwa sasa ni kama vile umepigwa teke la Van Damme, hali ya biashara ni ngumu, sasa unapoendekeza majungu na na fitna katika kipindi hiki inakuwa ni sawa na kuchinja ng’ombe mzima kwa oda ya maini”, alisema Jose Mara.

Kwasasa Jose Mara anaendelea kufanya vema na bendi yake kupitia wimbo wao mpya “Dunia Simama”.

No comments