JOSE MOURINHO ATAMANI KUZEEKEA MANCHESTER UNITED

KOCHA wa Manchester United, Jose Mourinho ni kama anatamani kuzeekea kwenye kikosi hicho baada ya kusema kwamba angependa kukinoa kikosi hicho kwa muda wa miaka 15 zaidi, lakini akakiri kuwa kumpiku Sir Alex Ferguson ni jambo ambalo haliwezekani.

Kocha huyo raia wa Ureno aliwasili kwenye klabu hiyo ya Old Trafford msimu uliopita na kuiwezesha kutwaa mataji matatu ambayo ni ya Ligi ya Europa, Kombe la EFL na Ngao ya Jamii ikiwa ni msimu wake wa kwanza.

Kwa sasa Mourinho mwenye umri wa miaka 54, amepania kuhakikisha anafikisha miaka 15 akiinoa man United na anakiri ili aweze kufikisha muda huo ni lazima mafanikio yawepo.


“Nipo tayari kwa ajili ya hilo. Nipo tayari kwa ajili ya miaka 15 ijayo, naweza kusema hivyo, kwanini isiwe hivyo?” Mourinho aliuambia mtandao wa ESPN FC.

No comments