JOSE MOURINHO AWEKA MEZANI PAUNI MILIONI 100 KUONGEZA SILAHA MBILI OLD TRAFFORD ... Ivan Perisic yuko njiani


JOSE MOURINHO ameripotiwa kujiandaa kutumia pauni milioni 100 kuongeza wachezaji wengine wawili wapya katika kikosi chake kiangazi hiki.

Gazeti la Mirror limedai kuwa Manchester United iko tayari kuweka dau la pauni milioni 60 kwa ajili ya kiungo Eric Dier wa Tottenham.

Kwa upande mwingine, The Independent limeripoti kwamba Mourinho atakamilisha uhamisho wa Ivan Perisic wiki ijayo kutoka Inter Milan, dili linaloweza kugharimu kati ya pauni milioni 45 na 50.

No comments