JOSEPH OMOG ASEMA AMEANZA KUIONA SIMBA YA MATUMAINI

KOCHA wa Simba, Joseph Omog amesema kwamba sasa baada ya wachezaji wake waliokuwa na timu ya taifa “Taifa Stars” kujiunga na kambi hiyo, kuna kitu kinaanza kuonekana.

Amesema, anataka kuwa na wachezaji wake wote kwenye kambi hiyo lakini kwa bahati mbaya ameambiwa kuwa kuna wachezaji wanne watajiunga na wenzao baada ya Simba Day.


“Nimeambiwa kuwa kuna wachezaji watajiunga na timu baada ya Simba Day kwani kuna mambo yanakamilishwa.

Mimi pia sina presha kwani kikosi changu chote cha zamani ninacho ukiacha wachezaji wachache sana,” amesema Omog.  

No comments