JUSTIN BIEBER ADAKWA NA POLISI KWA KUENDESHA GARI HUKU AKIONGEA NA SIMU

MWANAMUZIKI Justin Bieber ameingia kwenye mikono ya polisi baada ya kukamatwa akiwa anaendesha gari huku akiwa anaongea na simu, kitu ambacho ni kinyume na sheria nchini Marekani, hasa katika jiji la Los Angeles.

Bieber amekuwa na historia ya utukutu na hivi karibuni akikiri kujutia vituko vyake na kuanza maisha upya akiwa mtu mwema baada ya kuchoshwa na mashitaka ya polisi mara kwa mara.

Baada ya kunaswa na polisi alilazimika kulipa faini ya dola za Marekani 160 kama sheria za Los Angeles zinavyotaka.


Justin Bieber alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Serena Gomez kabla ya wawili hao kutengana huku chanzo kikubwa kikiwa ni Bieber kutopenda kutulia.

No comments