Habari

JUUKO MURSHID HUYOO AFRIKA KUSINI

on

BEKI wa kati wa timu ya taifa
ya Uganda “The Cranes”, Juuko Murshid anaweza kujiunga na miamba ya soka nchini
Afrika Kusini, klabu ya Orlando Pirates.
Mtandao wa habari za michezo
nchini Uganda wa Kawowo Sports umeandika kwamba una habari za kuaminika kwamba
Juuko anakwenda kujiunga na watemi hao wa soka barani Afrika wakati wowote.  
Mtandao huo umeandika kwamba
beki huyo mwenye umri wa miaka 23 anaweza kuondoka mwishoni mwa wiki hii kwenda
“Bondeni” kwani alishaonyesha nia ya kuondoka Simba tangu msimu uliopita.

Imedaiwa kuwa safari ya Juuko
ilichelewa kutokana na matatizo ya Visa lakini sasa mlinzi huyo wa zamani wa
klabu za Bunamwaya na SC Victoria mamo yake ni kama yameiva.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *