JUVENTUS NA CHELSEA ZATUNISHIANA MSULI KWA ALEX SANDRO


JUVENTUS imempa Mbrazil Alex Sandro ofa ya mshahara wa pauni 84,000 kwa wiki ili asaini dili jipya, wakati Chelsea ikiwa tayari kulipa dau la pauni milioni 61, ambalo ni rekodi ya dunia kwa mchezaji anayecheza nafasi ya beki, baada ya dau lake la pauni milioni 52 kukataliwa mwezi uliopita.

Klabu hiyo ya Serie A inafanya kila iwezalo kumbakisha beki huyo wa kulia mwenye umri wa miaka 26, lakini ofa hiyo ya Chelsea iliyoripotiwa kwenda sambamba na mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki inaweza kuzima jitihada zao.

Kwa mujibu wa gazeti la Evening Standard, Juventus inajaribu kumshawishi Sandro kubaki angalau kwa msimu mmoja, ikitumia maombi ya kutaka kumsajili staa wa Real Madrid, Danilo – rafiki yake wa karibu aliyecheza naye Porto kuziba nafasi ya Dani Alves.

No comments