JUVENTUS SASA YATANGAZA OFA KWA EMRE CAN WA LIVERPOOL

TIMU ya Juventus nayo inaonekana kuwa miongoni mwa timu zinazotaka kuibomoa Liverpool, baada ya kutangaza kutoa ofa wakimtaka nyota wao, Emre Can.

Mtandao wa Tuttosport, umesema Juventus watatuma ofa ya zaidi ya Euro milioni 30 ili kuhakikisha wanapata huduma ya kiungo huyo kuanzia majira haya ya joto.


Jarida hilo lilieleza pia kwamba huenda Can akaipokea ofa hiyo kwa mikono mwili ili aweze kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara jambo ambalo litamhakikishia namba kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ujerumani.

No comments