JUVENTUS YAIBUKA NA KUTIBUA HARAKATI ZA USAJILI WA MATIC KWENDA MANCHESTER UNITED


Diego Costa na Nemanja Matic sio sehemu ya kikosi cha Chelsea kwenye ziara yao ya Asia kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya.

Costa hakurejea Chelsea kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya yaliyoanza wiki hii ambapo alipewa ruhusa ya kutanua likizo yake ili apate wasaa wa kumaliza mazungumzo yake na Atletico Madrid ambayo inataka kumsajili.

Matic amekuwa mazoezini  Chelsea lakini muda mwingi alikuwa akifanya mazoezi ya peke yake na jina lake halikuorodheshwa na  Antonio Conte kwenye safari ya bara la Asia.

Juventus ambayo ilijaribu kumsajili kiungo huyo wa Serbia mwaka jana, imeibuka tena kutaka saini ya Matic ambaye anawaniwa na Manchester United.

Ni wazi kuwa Conte atapendelea kumuuza Juventus kuliko kwa mahasimu wao wa Premier League - Manchester United.

Matic amekuwa akitaka kwenda  Old Trafford lakini uhusiano wa vilabu hivyo viwili uliingia doa baada United kuipuku Chelsea katika usajili wa Romelu Lukaku kutoka Everton.

No comments