JUVENTUS YAIPIGA BAO LA KISIGINO CHELSEA


WINGA kinda anayetakiwa na Chelsea, Federico Bernardeschi yu mbioni kuondoka Fiorentina na kujiunga na mabingwa wa Italia, Juventus.


Kwa mujibu wa gazeti la Corriere dello Sport, Juve inatarajiwa kumnasa winga huyo kwa dau la pauni milioni 35 pamoja na kutoa mchezaji mmoja kati ya Stefano Sturaro na Tomas Rincon.

No comments