JUVENTUS YAKARIBIA KUMNASA MRITHI WA DANI ALVES


MTANGAZAJI wa televisheni ya Sky Sport, Gianluca Di Marzio amedai kwamba mabingwa wa Serie A, Juventus wanaongoza mbio za kuwania saini ya beki wa kulia wa Real Madrid mwenye umri wa miaka 25, Danilo (pichani juu), ambaye anaweza kupatikana kwa pauni milioni 17.5.

Wakala wa beki huyo wa kimataifa wa Brazil anayefuatiliwa pia na Chelsea tangu Januari, amejipanga kufanya mazungumzo zaidi na Juventus inayotaka kuziba nafasi ya Dani Alves aliyethibitisha kuwaacha mabingwa hao wa Italia.


Danilo alijiunga na Madrid akitokea Porto kwa dau la karibu pauni milioni 26 mwaka 2015, lakini alikuwa katika mahangaiko ya kupata namba ya kudumu chini ya Zinedine Zidane msimu uliomalizika.

No comments