JUVENTUS YASHUSHA "KITASA" MBADALA WA DANI ALVES

UHAKIKA ni kwamba Dani Alves, beki mwenye uwezo mkubwa wa kuzuia mashambulizi na wakati huohuo kupanda na kusaidia kutia hekaheka kwenye lango la mpinzani hatakuwepo katika kikosi cha Juventus.

Lakini miamba hao wa Italia wamesema kwamba haina noma wemeshusha mtu mmoja matata zaidi ambaye akiwa katika kiwango chake atawasahaurisha kabisa kuondoka kwa Alves.

Habari zinasema kwambna Juventus wamemsasjili Mattia De Sciliglio ambaye amehama kutoka klabu nyingine kubwa ya AC Milan.

Mchezaji huyo mwenyewe amesema kwamba baada ya kutemwa huko alikuwa anataka kuwaonyesha kwamba ana uwezo mkubwa kuliko inavyofikiriwa.

“Kwa hakika nimefarijika sana kupata nafasi katika klabu hii kubwa barani Ulaya na duniani kote, nataka kuonyesha kuonyesha uwezo wangu wa kuisaidia timu hii,” amesema katika mkutano wake wa kwanza na wanahabari.

Amesema kwamba kupata nafasi katika timu kubwa kama hiyo ni fursa adimu na ameapa kwamba atafanya kila analoweza kuhakikisha kwamba Juventus inakuwa katika ubora wake uleule.

De Sciglio amehamia Juventus wakati ambao anahitajika zaidi kwani walikuwa hawajampata mbadala wa Dani Alves aliyeondoka baada ya kuwatumikia kwa msimu mmoja tu.

Nimekuja hapa kufanya kazi moja kubwa, kupambana na kuhakikisha kwamba timu inapata mafanikio makubwa. Hii si nafasi ambayo kila anayeitaka anaipata. Juventus ni timu kubwa na kucheza hapa ni jambo adimu sana,” amesema mchezaji huyo.

No comments