JUVENTUS YAWATOLEA MACHO MASTAA WAWILI WA LAZIO

MABINGWA wa Serie A, Juventus wameelekeza jicho la usajili ndani ya klabu ya Lazio na tayari wameonyesha dhamira ya kunasa saini ya nyota wawili kwa mpigo.

Keita Balde Diao na Sergej Milinkovic-Savic ndiyo walioingia katika kurunzi la usajili wa kibibi kizee cha Tulin ambapo sasa mazungumzo kwa ajili ya kuwatia mkononi yanakwenda vyema.

Hatua ya Juve kuwataka nyota hao inatokana na ukweli kuwa huenda wakawakosa baadhi ya nyota wao muhimu, akiwepo Paulo Dybala anayehusishwa kutakiwa na klabu ya Barcelona.

Taarifa kutoka ndani ya Juve zinasema kuwa Keita Balde Diao na Sergej Milinkovic-Savic tayari wameanza mazungumzo ya mwisho.

 “Tunahitaji wachezaji wenye kiwango kama cha akina Keita Balde Diao na Sergej Milinkovic-Savic kwa sababu ni watu wa kiwango,” ilielezwa katika tovuti ya klabu ya Juventus.

Bianconeri tayari wana uhakika wa mwanandinga kama Federico Bernardeschi, Mattia De Sciglio, Douglas Costa, Wojciech Szczesny na Rodrigo Bentancur.


Hata hivyo Juve wanahitaji kuongeza mbio za usajili wa Balde Keita Diao kwani baadhi ya klabu nyingi za barani Ulaya nazo zinasaka saini ya nyota huyo, ambapo pia Sergej Milinkovis-Savic naye anmawindwa vikali na klabu kama Manchester City na PSG.

No comments