KAMUSOKO AANZA BALAA MAZOEZINI YANGA SC

KIUNGO Mzimbabwe Thabani Scara Kamusoko ambaye Jumatano iiliyopita aliongeza mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga baada ya mavutano na uongozi kwa takribani mwezi mmoja, ameanza balaa lake mazoezini.

Baada ya kusaini mkataba huo mpya utakaomfanya adumu Jangwani hadi Julai 2019, Kamusoko alijiunga na mwenzake kwa mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya.

Mchezaji huyo mtaalamu wa kugawa pasi alisajiliwa Yanga SC mwaka 2015 kutoka FC Platinums ya kwao Donald Ngoma ambaye naye tayari ameongeza mkataba Jangwani.

Kamusoko pamoja na wachezaji wenzake walifanya mazoezi ya kupasha na kunyoosha viungo baada ya hapo waliingia kwenye hatua nyingine ya kukimbia katika mashine maalum na kunyakua vitu ili kujiweka sawa kwa ajili ya msimu ujao.

Meneja wa timu hiyo, Hafidhi Saleh alisema kwa mijubu wa ratiba ya kocha wataendelea na mazoezi ya gym hadi mwishoni mwa wiki hii ili kuwaweka sawa wachezaji wao kabla ya kuanza rasmi harakati za kujenga kikosi cha ushindi.

“Kwa mijibu wa Lwandamina wachezaji watafanya mazoezi ya gym kwa muda wa wiki mzima kabla ya kurejea uwanjani au ufukweni lengo kubwa ni kuiweka miili ya wachezaji katika hali ya utayari kwa kuwa walikuwa mapunzikoni,” alisema.


No comments