KAMUSOKO AJIFUA BILA KOCHA NYUMBANI KWAO ZIMBABWE

KIUNGO wa Yanga, Thaban Kamusoko ameanza mazoezi ya kupasha misuli kivyake bila kusubiri program ya kocha mkuu wa timu hiyo, George Lwandamina kujiandaa kwa msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.

Kamusoko kwa sasa yupo nchini kwao kwa mapumziko lakini hajaachia mwili kwani amekuwa akiendelea kujifua ili kujiweka fiti zaidi.

Kupitia ukurasa wake kwenye mtandao wa kijamii, Kamusoko aliweka video akiwa anajifua peke yake uwanjani nchini Zimbabwe na kuandika kuwa “ikiwa unajiona upo vizuri kwenye kazi yako huwezi kubweteka hivyo lazima uzidishe vionjo katika hilo.”

Kamusoko ambaye ana uwezo wa kucheza viungo alisajiliwa Yanga katika misimu miwili iliyopita ya Ligi Kuu Bara akitokea Platnumz ya Zimbabwe.


Hata hivyo Kamusoko anatarajia kurejea nchini wakati wowote kuungana na wachezaji wenzake kujiandaa na msimu mpya wa Ligi.

No comments