KELVIN SABATO ACHEKELEA KUONGEZWA TIMU YA TAIFA

STRAIKA wa Majimaji ya Songea ambae ni maarufu pia kwenye mashindano ya Ndondo Cup, Kelvin Sabato ameitwa kukiongezea makali kikosi cha Taifa Stars.

Baada ya kutoka Afrika Kusini kushiriki michuano ya Cosafa ambayo imeshika nafasi ya tatu, Taifa Stars itakuwa na kibarua cha kuwania nafasi ya kucheza michuano ya Chan dhidi ya Rwanda Julai 15.

Sabato amefurahia kuitwa kwake na kusema ni sehemu ya ndoto zake kuchezea timu ya taifa pia nyota huyo amegusia kucheza kwake Ndondo.

“Nimefurahia sana kuitwa timu ya taifa na nitajitahidi kuonyesha kuwa Mayanga hajakosea kuniongeza kwenye kikosi chake,” alisema Sabato.


Sabato aliyekuwa akihusishwa kujiunga na Simba kipindi hiki cha usajili, anachezea timu ya Stimosha ambayo imefanikiwa kutinga hatua ya 16 bora katika mashindano ya Ndondo Cup.

No comments