KIBAHA CARNIVAL BAND SASA KUTUMBUIZA "NYUMBANI" PEKEE

BENDI ya Kibaha Carnival inajiandaa kuanza kukatisha maonyesho yake katika kumbi za nje ambapo itabaki kutumbyiza kwenye ukumbi wao wa nyumbani  wa Kibaha carnival Garden pekee.

Iddy Moro ambaye ni kiongozi wa jukwaa amemweleza mwandishi wa habari hizi kuwa wamefikia maamuzi hayo baada ya kuitangaza bendi vya kutosha kwa kufanya shoo katika kumbi mbalimbali za nje.

“Kuanzia mwezi ujao tutakuwa tukirindimisha burudani ndani ya Kibaha Carnival Garden pekee, tunawakaribisha mashabiki wetu wote tufurahi pamoja,” amesema Iddy.


Iddy amesema kuwa hata hivyo wataendelea kupokea mialiko ya kutumbuiza kwenye shoo maalum za mara mojamoja pamoja na kwenye sherehe mbalimbali zitakapotokea.

No comments